ILANI INATOLEWA kwamba Mkutano Mkuu wa Mwaka wa wanahisa wa Telesecurity Company Limited utafanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Bamaga -Mwenge ktk makutano ya barabara mpya ya Bagamaoyo na Sinza Mkoa wa Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 19 Novemba, 2022 mnamo saa 3:30 asubuhi kwa madhumuni yafuatayo:
- Kufungua Mkutano Mkuu
- Kusoma Ilani ya kuitisha Mkutano Mkuu
- Kupitisha Agenda za Mkutano Mkuu
- Semina fupi kwa Wanahisa
- Kudhibitisha kumbukumbu za Mkutano za Mkuu wa Mwaka uliofanyika tarehe 20/11/2021
- Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika tarehe 20/11/2021
- Taarifa ya Mwenyekiti
- Kupokea na kupitisha taarifa ya mahesabu yaliyokaguliwa kwa mwaka wa fedha ulioisha 31/12/2021 pamoja na taarifa ya Wakurugenzi na Wakaguzi wa hesabu
- Kuzingatia kwamba wakaguzi wan je wataendelea kukagua hesabu kwa mujibu wa kifungu cha 170(2) cha sheria ya makampuni
- Kupokea na kupitisha mapendekezo ya Wakurugenzi kuwa hakutakuwa na gawio la pili kwa mwaka wa fedha ulioishia 31/12/2021
- Kuhidhinisha malipo ya Wakurugenzi kwa mwaka unaofuata-2023
- Kufanya uchaguzi wa Wakurugenzi wapya
- Shughuli nyingine yeyote ile pale ambapo taarifa inayostahili itakuwa imepokelewa mapema
- Kufunga Mkutano Mkuu
Kwa Amri ya Bodi ya Wakurugenzi
Leonard Laibu
Katibu
Maelezo:
Fomu ya uwakilishi inapatikana kwenye matawi yote ya Telesecurity na kwenye tovuti www.telesecurity.co.tz. Fomu ya uwakilishi iliyojazwa inatakiwa kufikishwa/kutumwa Makao Makuu sio chini ya masaa 48 kabla ya Mkutano Mkuu, la-sivyo fomu hiyo haitatambulika.
Wanahisa wafike na kadi itakayowatambulisha kama kadi ya uanachama, leseni ya udereva, kitambulisho cha mpiga kura au kitambulisho cha Taifa.