Telesecurity Co Ltd

Taarifa imetolewa kwamba Mkutano Mkuu wa ishirini na moja (21) wa mwaka wa wanahisa wa Kampuni ya Telesecurity utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 29 Novemba, 2025 kuanzia saa tatu na nusu (3:30) asubuhi katika Ukumbi wa Ngome uliopo Afrika Sana – karibu na TRA Mwenge mkoa wa Dar es Salaam kujadili dondoo zifuatazo:

  1. Kufungua Mkutano;
  2. Kusoma taarifa ya Mkutano Mkuu;
  3. Kuthibitisha Kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa ishirini (20) wa mwaka uliofanyika tarehe 22 Novemba, 2024;
  4. Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa ishirini ishirini (20) uliofanyika tarehe 22 Novemba, 2024;
  5. Taarifa ya Mwenyekiti ya mwaka 2024;
  6. Kupokea, na kupitisha taarifa ya Mahesabu yaliyokaguliwa kwa Mwaka wa fedha ulioishia 31/12/2024 pamoja na taarifa ya Wakurugenzi na Wakaguzi wa Hesabu.
  7. Kuidhinisha ada ya Wakurugenzi kwa mwaka unaoishia 2025
  8. Kupokea na kupitisha mapendekezo ya Wakurugenzi kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa gawio la mwaka.
  9. Kuidhinisha malipo ya Wakurugenzi kwa mwaka 2025;
  10. Mengineyo kwa idhini ya Mwenyekiti;
  11. Kufunga Mkutano.

                                    Kwa Amri ya Bodi ya Wakurugenzi

Hussein Nguvu

                       KATIBU

MAELEZO:

Fomu ya Uwakilishi inapatikana kwenye matawi yote ya Telesecurity na kwenye Tovuti www.telesecurity.co.tz.  Fomu ya uwakilishi iliyojazwa inatakiwa kufikishwa/kutumwa Makao Makuu ya Kampuni kabla ya Mkutano Mkuu.

Wanahisa wafike na kadi itakayowatambulsiha kama Kadi ya Uanachama, Leseni ya Udereva, Kitambulisho wa Mpiga Kura au Kitambulsiho cha Taifa.